Muongozo wa ndani ya FORVAC juu ya COVID-19
Mnamo Januari 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuzuka kwa ugonjwa mpya wa virusi vya corona katika Mkoa wa Hubei, Uchina kuwa ni ugonjwa wa dharura kwa jamii unaotia wasiwasi kimataifa. Kama tulivyoona kupitia vyombo vya habari, ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) unaenea haraka kwa nchi zingine kote ulimwenguni.