Mikakati yetu
FORVAC inazingatia katika kuendeleza mnyororo wa thamani katika mazao ya misitu kama mbao, mkaa, na mazao mengine ya misitu yasiyo timbao kwenye misitu ya asili ya jamii na vijiji katika wilaya za programu. Programu hii pia inasaidia katika usimamizi wa Sheria za misitu, ambayo huleta maendeleo endelevu ya misitu ya jamii na vijiji na kuboresha biashara ya mbao, mkaa na mazao mengine ya misitu yanayovunwa kihalali katika maeneo ya programu. Mfumo wa kisheria na sera unapaswa kuboreshwa na kuoanishwa ili kuongeza usimamizi endelevu wa misitu na taratibu za kibiashara. Aidha, jukumu la sekta binafsi ni kubwa katika kukuza uchumi unaotokana na minyororo ya thamani ya mazao ya misitu. Mbali na jamii, mashirika ya sekta binafsi, hususani wafanyabiashara wanaojishughulisha na uvunaji wa bidhaa za misitu na zisizo za misitu, usindikaji, usafirishaji na uuzaji zina jukumu kubwa katika utekelezaji wa shughuli za FORVAC.