Timu yetu
Peter O'Hara
Kiongozi Mshauri Mwelekezi (CTA)
Peter O'hara hufanya kazi kama Kiongozi wa Timu ya FORVAC, kusimamia na kuongoza timu ya kiufundi (TA), ana jukumu la kupanga na kutekeleza shughuli za programu, kuangalia na kutathmini na kutoa ripoti. Peter O'hara ana jukumu la kuunganisha washirika wa kitaifa na kimataifa na wadau wengine wa programu. Sambamba na maendeleo ya mnyororo wa thamani ya misitu, yeye pia anatoa ushauri juu ya sera, sheria za misitu na masuala yanayohusiana na uhalalishwaji wa mbao.
Emma Nzunda
Mratibu wa Kitaifa wa Programu (NPC)
Emma Nzunda anamajukumu ya kusimamia rasilimali zitolewazo na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kuwa zinatumika ipasavyo na kwa ufanisi. Pia, anasaidia kuandaa mipango ya programu, utekelezaji na ufuatiliaji wa matokeo ya FORVAC kulingana na malengo yaliyopangwa. Nzunda e pia anaratibu na kuunganisha shughuli za programu ambazo zinatekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI).
Eric Mabewa
Meneja wa Fedha na Utawala (FAM)
Eric Mabewa anafanya kazi za kuratibu mipango ya kifedha, bajeti na kufuatilia matumizi ya fedha katika programu ya FORVAC. Pia anajukumu la kusimamia rasimali watu, mali za ofisi na mali nyingine zisizohamishika na usimamizi wa fedha wa kila siku na uandaji wa taarifa ya fedha. Eric Mabewa pia husimamia waratibu wa kongani zote katika masuala ya taarifa za fedha na ufuatiliaji.
Nette Korhonen
Afisa wa Kimataifa
Nette Korhonen anafanya kazi kama Afisa wa Kimataifa na anasaidia timu ya kiutendaji (TA) katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za programu hususani kwenye upande wa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya programu. Vilevile anasimamia Mfumo wa usimamizi wa taarifa (MIS) na mitandao ya kijamii ya FORVAC.
Marcel Mutunda
Mtaalam wa Usimamizi wa Misitu (FME)
Marcel Mutunda anafanya kazi kama Mtaalamu wa Usimamizi wa Misitu wa FORVAC. Majukumu yake ni pamoja na kuendeleza Usimamizi wa Misitu ya Jamii na vijiji (CBFM) na uendelezaji wa minyororo ya thamani inayopatikana kutoka kwa vijiji na wilaya zilizopo kwenye eneo la programu. Pia, anasimamia na kuongoza shughuli za kongani za FORVAC ambazo ziko katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Lindi na Ruvuma.
Eustack Bonifasi
Mratibu wa Kongani (CC), Mkoa wa Lindi
Eustack Bonifasi anasimamia utekelezaji wa shughuli za FORVAC katika wilaya tatu, ambazo ni Liwale, Ruangwa na Nachingwea zilizopo mkoa wa Lindi. Anaandaa mipango kazi na bajeti za shughuli za kongani ya Lindi na hutoa taarifa na mwongozo katika ngazi za vijiji na wilaya juu ya mbinu za utekelezaji, fursa zilizopo na faida za usimamizi wa hifadhi za misitu ya jamii, vijiji na minyororo ya thamani inayohusiana.
Petro Masolwa
Mratibu wa Kongani (CC), Mkoa wa Ruvuma
Petro Masolwa anasimamia utekelezaji wa shughuli za FORVAC katika wilaya tano, ambazo ni Namtumbo, Songea, Nyasa, Mbinga na Tunduru zilizopo mkoa wa Ruvuma. Anaandaa mipango kazi na bajeti ya shughuli za kongani ya Ruvuma na hutoa taarifa na mwongozo katika ngazi za vijiji na wilaya juu ya mbinu za utekelezaji, fursa zilizopo na faida za usimamizi wa hifadhi za misitu ya jamii, vijiji na minyororo ya thamani inayohusiana.