Tunapofanya kazi
Sehemu ambapo programu ya FORVAC inatekelezwa imegawanywa katika kongano tatu kama ifuatavyo
- Kongano ya Tanga: wilaya za Handeni na Kilindi zilizopo Tanga, wilaya ya Mpwapwa iliyopo mkoa wa Dodoma na wilaya Kiteto iliyopo mkoa wa Manyara.
- Kongano ya Lindi: wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea.
- Kongano ya Ruvuma: wilaya za Namtumbo, Songea, Mbinga ,Nyasa na Tunduru
Programu hii pia inashughulikia ujengaji wa uwezo na maendeleo ya sera katika ngazi za mikoa na kitaifa. Makao makuu ya FORVAC yapo mjini Dodoma. Ofisi za kongano zipo wilayani Kilindi (Kongano ya Tanga), Ruangwa (kongano ya Lindi) na Songea (kongano ya Ruvuma)